Mamma Mia...
Mustafa Hassanali kuhamasisha uzazi salama nchini Tanzania
Maonyesho ya bure ya kwanza ya mavazi kufanyika tarehe 5 Machi
Fedha zaidi zahitajika toka serikalini kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi
Yale maonyesho ya mavazi yajulikanayo kama ‘mamma mia’ yenye nia ya kuhamasisha uzazi salama, sambamba na sherehe za miaka 50 ya uhuru Tanzania, na miaka mia moja ya siku ya mwanamke duniani , kwa kushirikiana na shiriki lisilo la kiserikali la utepe mweupe ‘White Ribbon Alliance’ na ‘Vodacom Foundation’, yazinduliwa rasmi.
Akizungumza katika uzinduzi huo, mbunifu wa mavazi, aliyejipatia umaarufu kitaifa na kimataifa, Mustafa Hassanali amesema “ntazindua toleo langu jipya la ki-afrika katika maonyesho haya ya ‘Mamma Mia’ siku ya tarehe 4 na tano mwezi Machi hapahapa jijini Dar es salaam, na nategemea kupata ushirikiano wa watu wote, katika kuhamasisha uzazi salama kwa msaada wa shirika la utepe mweupe”
‘Mamma Mia’ ni jukwaa la maonyesho ya mavazi ambalo limelengwa mahsusi katika kusambaza ujumbe kuhusu uzazi salama, litafanyika tarehe nne mwezi machi, katika hoteli ya ‘Moevenpick Royal Palm’ kuanzia saa mbili na nusu usiku, na onyesho jingine kwa siku ya Jumamosi ya tarehe tano kuanzia saa tisa na nusu jioni, katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
“nimefurahi sana kuwa wa kwanza kuandaa onyesho la mavazi la bure nchini kwa siku ya tarehe tano, ambalo madhumuni yake sio tu kuhamasisha uzazi salama, bali pia kuifanya tasnia ya ubunifu wa mavazi na mitindo iweze kufikiwa na wengi pale katika viwanja vya Mnazi Mmoja.” Alieleza Hassanali
Akizungumza kuhusu ‘Mamma Mia’ ni jina lililotokana na wimbo uliovuma sana katika miaka ya 80 na kundi la ‘ABBA’, ambapo mia inasimama kuiwakilisha sarafu ya shilingi mia , na miaka mia moja ya ya siku ya mwanamke duniani, Mustafa anaongeza kuwa, “kwa kila atakae kuja kuangalia shoo, atatoa shilingi mia moja, si kwa maana nyingine bali ni kama mchango wake katika kuhamasisha uzazi salama nchini”
Akiongezea katika suala zima la uzazi salama, mratibu wa Taifa wa Muungano wa jumuiya ya utepe mweupe na uzazi salama nchini, Bi Rose Mlay amesema kuwa, toka mwaka 2004, wamekuwa mstari wa mbali katika kuhamasisha and kuiomba serikali kuongeza fungu katika bajeti ya sekta ya afya na uuguzi, ili kupunguza vifo vitokanavyo na matatizo ya uzazi.
“mpaka sasa, ni asilimia 51 tu ya wanawake wote Tanzania , ndio wanaojifungua chini ya usimamizi na kusaidiwa na wataalamu wa afya, na sababu kuu ya hili ni upungufu wa vifaa na wafanyakazi wa afya katika sekta ya uzazi kwa mikoa mingi ya pembezoni mwa Tanzania, hii sio nzuri na Haikubaliki, kwani kila mwanamke ana haki ya kujifungua salama chini ya wataalamu wa afya. Na ndio maana tunahamasisha uzazi salama.”aliongezea kusema Mama Mlay.
Msukumo wa hili hautawezekana bila ushirikiano kutoka watu na mashirika mbalimbali, ambapo Mamma mia kwa ushirikiano na shirika la utepe mweupe ( White Ribbon Alliance) pamoja na ‘Vodacom Foundation’ ikiwa na baadhi ya waliojitolea kusaidia hili ni pamoja na ‘Johns Hopkins Centre for Communication Programs in Tanzania’, The Citizen, ‘Uhuru one’, ‘Moevenpick Royal Palm Hotel’, Novamedia, Ultimate Security, Darling Hair na Image Masters.
Wabunifu wengine watakaoshiriki katika kampeni hizi ni pamoja na mshindi wa tuzo za ubunifu kutoka Zanzibar Farouque Abdella, Henrietta Ludgate na Minna Hepbum wote toka ‘London Fashion Week’, Uingereza.
Nukuu kwa Mhariri:
KUHUSU MUSTAFA HASSANALI
Mustafa Hassanali ni mbunifu mjasiriamali anaeamini katika ‘daima sitashindwa’ huku akitumia kipaji chake na ubunifu wake wa mavazi katika kuleta maisha bora ya sasa na ya baadae.
Kazi za mbunifu Mustafa zimekuwa zikithaminika na kuonyeshwa kimataifa, ambapo Mustafa alifanikiwa kuonyesha ubunifu wake katika nchi kama Angola ‘Angola Fashion Business’, FAFA (Festival of African Fashion and Arts in Kenya), Kameruni, Wiki ya Mitindo India 2009, Naomi Campbell’s fashion for relief 2009, Arise Africa Fashion Week 2009, Wiki ya mavazi Durban & Cape town, Vukani Fashion Awards Pretoria, Miss Ethiopia Beauty Pageant, Mediterranean Fashion Festival, Sicily, Italia, M’net Face of Africa, Msumbiji, Uganda, na Wiki ya Mitindo Kenya, ambayo kwa pamoja yamemletea heshima kubwa, ndani na nje ya nchi.
KUHUSU SHIRIKA LA UTEPE MWEUPE
Ni shirika la kimataifa lisilo la kiserikali, lenye nia ya kuleta mabadiliko katika suala zima la uzazi salama, kati ya mama na mtoto duniani kote.
Katika jamii nyingine, rangi nyeupe ina maana ya majonzi, na jamii nyingine, nyeupe in maana ya matumaini na uhai, hivyo basi utepe mweupe umetwaliwa kama kumbukumbu kwa wanawake wote waliofariki kwa mimba , na katika harakati za kujifungua.
Toka ilipoanzishwa mwaka 1999, shirika la utepe mweupe limekuwa likikuwa kwa kasi duniani kote, hadi kufikia kuwa na nchi wanachama 148 ambao wanapaza sauti zao kwa ajili ya wanawake na jamii zao kwa ujumla. Ambapo kwa sasa linaongoza katika kuyakabili majanga yanayotokana na vifo vya uzazi.
KUHUSU MUSTAFA HASSANALI NA SHIRIKA LA UTEPE MWEUPE.
Mustafa Hassanali, ni mbunifu wa mavazi anayeshirikiana kwa karibu sana na shirika hili, ambapo kwa pamoja waliwahi kufanya onyesho na Naomi Campbell lililofahamika kama ‘Naomi Cambpell’s fashion for Relief’ mwaka 2009, ambapo zilokusanywa kiasi cha dola 65,000.
Mustafa Hassanali, mwenye shahada ya udaktari, anaamini kwa moyo mkunjufu kabisa katika kutumia mitindo kama njia yakusaidia kuchangisha fedha, na kusambaza ujumbe wa masuala ya afya kwa jamii yote.
Kwa maelezo zaidi tembelea www.mustafahassanali.net
No comments:
Post a Comment