Thursday, 29 April 2010

The Ngoma Africa Band kuwasha moto 8-May 2008 Munich,UjerumaniShamra Shamra za Wold Cup 2010 zinaripuka kila Kona ya duniani

FFU wa The Ngoma Africa Band kutumbuiza Munich! Ujerumani.

Mahala: Pfarrheim,St.Joseph, Joseph Platz 1.M√ľnchen,Germany

Ile bendi mashuhuri ya mziki wa dansi uko ughaibuni,The Ngoma Africa band alimaarufu kwa majina ya kutisha tisha,kama vile FFU,wazee wa kukaanga mbuyu,
yenye maskani yao uko Ujerumani,watapereka mzuka wao wa dansi mjini Munich
au bayern Munchen,kusini mwa Ujerumani.ambako wamehalikwa kwenda kutumbuiza siku ya Jumamosi 8 may 2010,katika kusherekea "FIFA World Cup 2010" kwa mara ya kwanza mashindano ya kombe hilo kufanyika Afrika.

Jumuiya za mshirika mbalimbali yasio ya Kiserekali ,Kikiwemo chama cha urafiki kati ya wajerumani na tanzania,ndio walioandaa onyesho ilo uko Munich,ujerumani ya kusini,ambako ndipo mjio huo ndio makao makuu ya timu maarufu ya kandanda ya Bayern Muchen.

Washabiki wa kandanda na washabiki wa mziki wa mataifa mbali mbali watapata
bahati ya kujumuika na kujimwaga uwanjani kwa kusakata mziki wa dansi kutoka
kwao bendi ya "The Ngoma Africa Band".bendi ambayo imezoeleka na washabiki
kwa tabia za kuperekana puta na wa shabiki kwa kutumia mdundo wake wa dansi!

Ni juzi tu bendi hiyo mashuhuri iliachia singo CD yake mpya "Jakaya Kikwete 2010".
Kikosi cha Ngoma Africa band,kitarajiwa kutua mjini Munich kwa kazi moja tu!
nayo ni kuwapa burudani ya kukata na mundu washabiki!Burudani ya pata shika na nguo kuchanika,kila moja na wake!

Wakazi na washabiki wa Muchen aka Bayern Munich kaeni mkao wa kula
pia unaweza kusikiliza mziki wao at http://www.myspace.com/thengomaafrica

No comments: